TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

DC MBONEKO AWATAKA WAFANYABIASHARA WA MBAO, AMBAO BADO WAPO KAMBARAGE WAHAMIE CHAMAGUHA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye ziara eneo jipya la kuuza Mbao, lililopo Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wafanyabiashara wa kuuza Mbao, ambao bado wapo kwenye Soko la Kambarage Manispaa ya Shinyanga, wahamie mara moja kwenye eneo ambalo wametengewa na Serikali lililopo Chamaguha, kabla ya kuwachukulia hatua.

Mboneko alibainisha hayo jana, alipofanya ziara ya kutembelea kwenye eneo jipya la kuuza Mbao lililopo Chamaguha, na kupewa malalamiko kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara bado hawajahamia huko na kubaki Kambarage, na kuombwa awaondoe ili wafanye biashara eneo moja.

Alisema Serikali iliwaondoa wafanyabiashara kwenye Soko hilo la Kambarage, ambalo lilikuwa finyu na siyo rafiki kwao kufanyabiashara hiyo ya kuuza Mbao, na kuwatengea eneo zuri la Chamaguha, na kuwataka wale ambao bado wapo Kambarage watii maagizo ya Serikali. na kuhamie kwenye eneo hilo jipya.

“Naagiza wale wafanyabiashara wa Mbao, ambao bado wapo huko Kambarage, waondoke mara moja, waje huku Chamaguha kwenye eneo lao, watii maagizo ya Serikali,”alisema Mboneko.

Pia, aliwataka akina mama kuchangamkia fursa ya kuuza chakula kwenye eneo hilo jipya la kuuza Mbao Chamaguha, ili wajipatie kipato na kuendesha maisha yao.

Nao baadhi ya wafanyabiashara hao wa kuuza Mbao ambao wamehamie kwenye eneo hilo jipya, walisema wanasikitika kuona wenzao bado wapo huko Kambarage wakifanyabiashara, na kugoma kuhamia Chamaguha kwenye eneo ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya biashara hiyo, na kumuomba Mkuu huyo wa wilaya awaondoe huko.

 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa kwenye Soko jipya la kuuza Mbao lililopo Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wafanyabiashara wa kuuza Mbao.

Mfanyabiashara wa kuuza Mbao Ernest Nangale, akitoa malalamiko kwa Mkuu wa Wilaya, kuwa bado kuna wenzao wapo Soko la Kambarage na kumuomba awaondoe huko.

Wafanyabiashara wa kuuza Mbao katika eneo jipya la Chamaguha wakiendelea na shughuli zao.

Wafanyabiashara wa kuuza Mbao katika eneo jipya la Chamaguha wakiendelea na shughuli zao.

Wafanyabiashara wa kuuza Mbao katika eneo jipya la Chamaguha wakiendelea na shughuli zao.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.