TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

RAIS MAGUFULI AMTEUA DK. BASHIRU ALLY KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi (Picha kutoka Maktaba)

***
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuchukua nafasi ya Balozi Mhandisi John Kijazi aliyefariki dunia Februari 17,2021.


Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi na kwamba uteuzi huo unaanza rasmi leo Ijumaa Februari 26,2021 na ataapishwa kesho saa tatu asubuhi Ikulu jijini Dar es salaam