Header Ads Widget

MENEJA FEDHA BEVCO LTD ALIYESAKWA NA TAKUKURU KWA SIKU 6 ANASAWA ITILIMA -SIMIYU

Nembo ya TAKUKURU

Na Shinyanga Press Club Blog

Mmoja wa waliokuwa vigogo wa Kampuni ya uagizaji na uuzaji vinywaji vikali kutoka nje ya nchi (BEVCO Ltd), Joseph Rwegasira Samson ambaye alikuwa Meneja Fedha wa kampuni hiyo, amekamatwa na makachero wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) baada ya kutangaza kumtafuta Novemba 19, 2020.

Rwegasira ni mmoja wa watuhumiwa wanne wa kmapuni hiyo ambao wanatuhumiwa na makosa ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi wa zaidi ya Sh Bilioni 1.6, amekamatwa leo katika Kijiji cha Kinangw'eli wilayani Itilima mkoa wa Simiyu.

 Soma zaidi hapa chini taarifa iliyotolewa leo Novemba 24, 2020 kwa vyombo vya habari na Afisa Uhusiano TAKUKURU, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo.




Post a Comment

0 Comments