Header Ads Widget

74,862 WANAOISHI NA VVU HALMASHAURI YA SHINYANGA WAUNGANISHWA NA HUDUMA, DC MBONEKO AKEMEA WIZI WA DAWA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye maadhimisho ya Ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika leo Kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola wilaya humo.  

Na Marco Maduhu, Shinyanga 
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI Duniani katika Kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola wilayani humo. 

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko na kuhudhuriwa na Watendaji wa halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Hoja Mahiba, ambapo kilele cha maadhimisho hayo ni Desemba Mosi mwaka huu. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, DC Mboneko amewataka wananchi wasiwanyanyapae watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, bali washirikiane nao katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo. 

Amesema ugonjwa huo ni kama ugonjwa mwingine, hivyo siyo vyema kuwatenga watu wenye maambuzi hayo ya virusi vya ukimwi, na kuwataka wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujikinga na maambukizi mapya ya virusi hivyo. 

"Naombeni sana wananchi tuishi vyema na watu ambao wana maambukizi ya virusi vya ukimwi, tusiwanyanyapae, na pia mpime afya zenu na kujikinga na maambukizi mapya," amesema Mboneko. 

"Pia watu ambao mnaendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU muendelee kutumia, pamoja na wataalam muwapatie huduma stahiki na kwa wakati," ameongeza. 

Katika hatua nyingine Mboneko, amekemea wizi wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za kiafya, na kubainisha Serikali imekuwa ikisambaza dawa Za kutosha, lakini anashaghaa kusikia taarifa za uhaba wa dawa kuwapo kwenye baadhi ya hospitali. 

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Damas Nyansira, akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya UKIMWI wilayani humo, alisema kiwango cha maambukizi ni asilimia 3. 

Amesema katika halmashauri hiyo kuna jumla ya watu 74,862 wanaoishi na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na wamekwisha unganishwa na huduma ya tiba na matunzo, na kubainisha changamoto ambazo zinazowakabili ni vituo vichache vinavyotoa huduma za CTC, ambapo vipo 10 na mahitaji ni 20. 

Amebainisha changamoto nyingine ni ushiriki duni wa jamii na hasa wanaume katika suala la upimaji VVU, Ufinyu wa bajeti ya fedha kwa Wadau wa UKIMWI na Serikali kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za UKIMWI katika Halmashauri, pamoja na upungufu wa dawa za kufubaza makali ya VVU kwa watoto. 

Kwa upande wake mmoja wa wananchi ambaye anaishi na virusi vya ukimwi (jina limehifadhiwa), aliwataka wananchi kujenga tabia ya kupimwa afya zao na kuachana na mila potofu za kurogwa, ili kujitambua na kulinda afya zao, na watakaogundulika na maambukizi watumie dawa za kufubaza makali ili waishi miaka mingi. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya Ukimwi katika Kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola wilayani Shinyanga.
  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi. Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Damas Nyansira akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani humo.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maadhimisho ya ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya ukimwi yakiendelea.
Awali mkuu wa wilaya akikagua mabanda ya wajasiriamali, kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya akiendelea na zoezi la kukagua mabanda ya wajasiriamali, kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
DC Jasinta Mboneko, akipima uzito kwenye maadhimisho ya Ukimwi wilayani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, akipima afya kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja akipima afya kwenye madhimisho hayo ya Ukimwi.
Mwandishi wa habari wa ITV Mkoani Shinyanga, Frank Mshana, akipima afya kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, akizindua zoezi la utoaji dawa za minyoo pamoja na vitamini A kwa watoto wenye kuanzia miezi Sita hadi Miaka Mitano, kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi.
Zoezi likiendelea.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, kulia akiingia kwenye maadhimisho hayo ya Ukimwi, akiambatana na Jeshi la Jadi Sungusungu, kushoto ni Diwani mteule wa Kata ya Ilola Amos Mshandete.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo ya Ukimwi.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo ya Ukimwi.

Post a Comment

0 Comments