Header Ads Widget

PICHA: CHUO CHA MADINI DODOMA, KITUO CHA JEMOLOJIA VYATOA ELIMU KWA WANANCHI

Wananchi wakitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Kituo cha Jemolojia kwenye maonesho ya teknolijia na wekezaji mjini Geita

Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) na Chuo cha Madini Dodoma( MRI) vimeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya tatu ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya madini yanayoendelea katika uwanja wa kituo cha uwekezaji Bomba Mbili mjini Geita.

Taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Mgodi wa STAMIGOLD.
Wananchi wakipata elimu juu ya masualambalimbai kutoka kwa ofisa wa chuo cha madini Dodoma kwenye maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji mjini Geita
Wananchi wakipata ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwenye banda la kituo cha Jemolojia
Wafanyakazi wa kituo cha Jemolojia wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya teknolojia na uwekezaji mjini Geita

Post a Comment

0 Comments