Header Ads Widget

VYAMA VYA USHIRIKA 2,539 VYAFUTWA, WIZARA YA KILIMO YAPONGEZWA


 
Wizara ya Kilimo imepongezwa kwa uamuzi wa kuvifuta vyama vya ushirika 2,539 ambavyo vilikuwa na utendaji mbovu uliosababisha kero kwa wanaushirika nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo (03.08.2020) na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji ) Angellah Kairuki wakati alipohutubia wananchi wa Simiyu kwenye maonesho ya Nanenane ikiwa ni siku maalum ya kuhamasisha ushirika.

Amesema hatua hiyo ya wizara itawezesha wanaushirika ambapo ni wakulima, wavuvi na wafugaji kunufaika na kazi zao ndani ya ushirika .

“ Ninawapongeza sana Wizara kwa hatua mliyochukua ya kuvifuta vyama vya ushirika 2,539 kwa sababu ya kutofanya kazi iliyokusudiwa.” alisema Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki alisema katika kipindi cha 2018/2019 jumla ya viwanda 75 vimeanzishwa na vyama vya ushirika vinavyochata alizeti, chikichi,kutengeneza samani za majumbani,kuchakata pamba na mazao ya nafaka pamoja na usindikaji wa maziwa.

“Viwanda vinavyomilikiwa na vyama vya ushirika vimeongezeka kutoka viwanda 133 mwaka 2018 hadi kufikia viwanda 208 mwaka 2019” alisema Waziri Kairuki.

Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao (EGA) kuangalia namna bora ya kuweka mfumo shirikishi wa TEHAMA utakaoweza