TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

VYAMA VYA UPINZANI KUKUTANA NA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA DODOMA


Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Wadau wa siasa, vikiwemo vyama vya upinzani nchini Tanzania wanakutana kwa siku tatu mjini Dodoma. Mkutano huo wa siku tatu utakaoanza Oktoba 21-23 mwaka huu, utahudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na viongozi wengine wa serikali wakiwemo baadhi ya mawaziri.
Akithibitisha hilo, Msajili msaidizi wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Sixty Nyahoza ameiambia BBC kwamba, mbali na waziri mkuu na baadhi ya mawaziri, mkutano huo utahusisha pia wadau wote muhimu katika siasa vikiwemo vyama vya siasa, Azaki, waandishi wa habari na viongozi wa dini.

Kwa mujibu wa Katiba na sheria za Tanzania, Waziri mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo ndani ya bunge, lenye mamlaka ya kutunga na kurekebisha sheria mbalimbali za nchi.
 
SOMA HAPA ZAIDI ; CHANZO BBC SWAHILI