Header Ads Widget

SPIKA JOB NDUGAI AFUNGUA WIKI YA AZAKI DODOMA...ATEMBELEA BANDA LA HAKIRASILIMALI

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, (wa pili kulia), akiwa katika Banda la HakiRasilimali wakati wa ufunguzi wa wiki ya AZAKI Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja.

Na Marco Maduhu, Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amefungua rasmi wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI) Jijini Dodoma na kuzionya baadhi ya asasi kuacha kutumika kuchafua nchi.
Uzinduzi wa wiki hiyo ya Asasi za kiraia  umefanyika katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Ndugai amesema anatambua mchango mkubwa wa Asasi za kiraia hapa nchini, katika ukuaji wa maendeleo ya taifa na kuhudumia wananchi, na kuzitaka Asasi ambazo zinatumika vibaya kuichafua nchi na viongozi ziache mara moja.

"Serikali inatambua mchango wa asasi za kiraia hapa nchini, na tunaomba muendeleze miradi yenu kwa kutafuta fedha ndani na nje ya nchi, na kuzileta kwa ajili ya maendeleo ya Taifa," alisema Spika Ndugai.

Aidha ,alisema asasi la kiraia zimekuwa zikifika maeneo ambayo Serikali haiwezi kufika, na kuwahudumia wananchi katika makundi mbalimbali kutatua changamoto zao, wakiwemo watu wenye ulemavu, yatima na wajane.

Katika hatua nyingine Ndugai alisema, Ofisi ya Bunge itaendelea kushirikiana na asasi za kiraia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma Fredy Mwakibete ,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Busekelo, akiwa katika Banda la HakiRasilimali, amezipongeza Asasi za kiraia, kwa kazi nzuri ambazo wanafanya hapa nchini.

Alisema kutokana na kazi hiyo nzuri, kuna haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa kutenga fungu katika bajeti yake, na kuziwezesha Asasi za kiraia katika kuwahudumia wananchi.

Pia ameipongeza Taasisi ya HakiRasilimali, kwa kazi zao ambazo wanazifanya ya uziduaji katika Sekta ya Madini, Oil na Gesi, na hata kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya 2,000 kushiriki katika Sekta ya madini.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilima Rachel Chagonja, alisema bado kuna changamoto ya masuala ya mila na imani potofu, juu ya wanawake kushiriki katika masuala ya uziduaji hasa Sekta ya madini, na kuiasa jamii iachane na mila hizo, ili kuleta usawa wa kijinsia katika uwajibikaji.

Wiki hii ni wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI) hapa nchini, yenye kauli mbiu isemayo, "Azaki na Maendeleo" ambapo Spika wa Bunge Job Ndugai, kabla ya kuzindua, alitembelea mabanda mbalimbali ya Azaki, likiwemo la HakiRasilimali ambao wanajihusisha na masuala ya uziduaji kwenye Sekta ya madini, oil, na Gesi.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, akifungua wiki ya AZAKI Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wananchi wa Dodoma na Asasi za kiraia wakiwa katika ufunguzi wa wiki ya AZAKI Jijini Dodoma.


Baadhi ya viongozi wa Asasi za kirai wakiwa meza kuu, ambapo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja, ambao wanajihusisha na masuala ya uziduaji katika Sekta ya Madini, Oil na Gesi.

Awali Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, wapili kulia, akiwa katika Banda la HakiRasilimali wakati wa ufunguzi wa wiki ya AZAKI Jijini Dodoma, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja.

Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja, akielezea namna wanavyofanya kazi ya Uziduaji katika Sekta ya Madini,Oil na Gesi.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Omari Kigau, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi mkoani Tanga, akizungumza katika banda la HakiRasilimali na kuelezea umuhimu wa Azaki hapa nchini ikiwamo Taasisi ya HakiRasilimali.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa umma Fredy Mwakibete, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Busekelo akizungumza katika Banda la Taasisi ya HakiRasilimali na kuipongeza kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya katika masuala ya uziduaji katika Sekta ya Madini, Oil na Gesi.

Meya wa Jiji la Dodoma  Davis Mwamfupe (wapili kulia), akiwa katika Banda la HakiRasilimali, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja. akiwa na wanachama wa chama cha wachimbaji madini wanawake Tanzania (TAWOMA).

Mbunge wa Jimbo la Mlalo mkoani Tanga Rashid Shaghazi, akiwa katika Banda la HakiRasilimali.

Mbunge wa Jimbo la Maswa mkoani Simiyu Stanlaus Nyongo (wapili kulia) akiwa katika Banda la HakiRasilimali, kiushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja.

Viongozi Mbalimbali wakiendelea kumimika katika Banda la HakiRasilimali, kuona shughuli zao za Uziduaji katika Sekta ya Madini, Oil na Gesi.

Viongozi Mbalimbali wakiendelea kumimika katika Banda la HakiRasilimali, kuona shughuli zao za Uziduaji katika Sekta ya Madini, Oil na Gesi.

Awali Maandamano ya ufunguzi wa wiki ya Azaki yakitokea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma kuelekea katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Rachel Chagonja (katikati) akiwa ameshika Bango wakati wa matembezi ya maandamano kuelekea kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Wafanyakazi HakiRasilimali wakiwa kwenye maandamano.

Wafanyakazi HakiRasilimali wakiwa kwenye maandamano.

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Asasi za kiraia, mara baada ya kumaliza kuzindua wiki ya Azaki Jijini Dodoma.

Na Marco Maduhu, DODOMA.

Post a Comment

0 Comments