TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

SABABU CHATO KUPIGWA KALENDA KUWA MKOA NA RAIS SAMIA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakamilisha vigezo vitakavyoruhusu Chato kuwa Mkoa.

Akihutubia kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 Samia amesema iwapo vigezo vyote vitakamilika Serikali itatangaza kuanzishwa kwa mkoa huo."Bado (Chato) haijawa Mkoa.....kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia na vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jambo hilo”amesema.

Mchakato wa kuanzishwa kwa mkoa huo tayari umeanza kwa kujadiliwa na kupitishwa kwenye vikao vya ngazi ya wilaya na mkoa wa Geita.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI