Header Ads Widget

MAKAHABA,WALEVI, WAPIGWA MARUFUKU KUCHANGIA DAMU





SERIKALI ya Uganda kupitia Bodi ya Kuchangia Damu (UBTS), imesema kuanzia sasa haitawaruhusu walevi, makahaba na watu wenye mpenzi zaidi ya mmoja 'Wahuni' kuchangia damu kwa hiari.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Benki ya Damu ya Nakasero, Samuel Wante wakati akizungumza na Gazeti la Daily Monitor nchini humo na kueleza kuwa sababu kubwa ya kukataa damu kutoka kwenye makundi hayo ya wachangiaji, ni hasara ambayo serikali imekuwa ikiingia.


Amesema utafiti wa kitaalamu umebaini kwamba damu inayochangiwa na walevi, makahaba na watu wenye mpenzi zaidi ya mmoja, asilimia kubwa hukutwa na maambukizi ya magonjwa kama Ukimwi, Kaswende, Kisonono na magonjwa mengine ya zinaa pamoja na yale yanayoambukizwa kwa njia ya ngono zembe.


Ameongeza kuwa, gharama ya kuhifadhi damu hiyo, huwa ni kubwa ambapo mwisho hubainika kwamba haiwezi kutumika na hivyo kumwagwa, wakati tayari serikali inakuwa imeshaingia gharama katika kuitunza na kuisafirisha mpaka maabara kubwa kwa ajili ya vipimo.
 
 
SOMA ZAIDI CHANZO MALUNDE BLOG


Post a Comment

0 Comments