Header Ads Widget

SENSA YA MAJARIBIO KUANZA AGOSTI MWAKA HUU, MAKINDA ATOA TAHADHARI

Kamisa wa zoezi la sensa 2022. Mhe.Bi Anna Makinda akiongea katika ofisi ya katibu tawala mkoa wa Shinyanga kuhusu maandalizi ya majaribio ya zoezi la sensa 2021 
 
Na Mwandishi wetu, Shinyanga
Kamati ya Sensa ya taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wataanza utekelezaji wa zoezi la sensa ya majaribio kwa baadhi ya mikoa  nchini kuanzia Agosti mwaka huu ili  kujiandaa kikamilifu na zoezi la sensa ya Taifa mwakani.
 
Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Sensa ya mwaka 2022, Anna Makinda alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Tanzania inatarajia kufanya zoezi la sensa kwa awamu ya sita kwa mwaka 2022 ili kuweza kuwa na takwimu zitakazosaidia Serikali kufanya mipango yake vizuri, ambapo Serikali hufanya zoezi la sensa kila baada ya miaka 10 ili kuweza kujua idadi ya watu na makazi yao na kufahamu zaidi changamoto na hali ya maendeleo yao.

"Ofisi ya Taifa ya Takwimu itafanya zoezi sensa ya majaribio kuanzia Agosti, 2021 kwa mikoa itakayoteuliwa na ofisi hiyo ili kubaini changamoto kabla kadhaa ambazo wataalam wetu watazibainisha na kuzifanyia kazi vizuri ili kuweza kufanya zoezi rasmi la sensa la mwaka 2022 kuwa na ubora zaidi.

"Majaribio ya sensa ya mwaka 2021 yatatumia zaidi mfumo wa Tehama kwa ajili ya kwenenda na teknlojia ili kuwapatia wadau urahisi wa kuweza kutumia taarifa za takwimu vizuri.

"Licha ya kuwepo hali ya ugonjwa wa UVIKO-19,Ofisi ya Taifa ya Takwimu itazangatia miongozo ya wizara ya afya katika utekelezaji wa sensa ya majaribio. Pia ni wakati muhimu kwa watanzania wote kupata chanjo kwa ajili ha UVIKO -19,"
alisema Makinda.

Anna Makinda alisisitiza kuwa ofisi ya Taifa ya Takwimu itatumia vyombo vya habari ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimi wa zoezi la sensa na ushiriki wao ili kuweza kuisadia serikali katika mipango mbalimbali ya maendeleo kwe sekta zote.

"Tanzania iko katika uchumi wa kati na muhimu sana kuwa na takwimu ili kusaidia kujua mahitaji ya taifa kwa kila sekta na kuweka mipango ya serikali vizuri," alisema.

Naye Afisa Mawasiliano wa ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir alisema kuwa huu ni wakati muhimu kwa mahitaji ya ndani ya takwimu kwa mpango ya serikali na hata jumuiya za kikanda ili kuweza kuwa na takwimu zitakazosaidia mipango ya maendeleo.

Kwa upande wake
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Zuena Omary alisema mkoa huo uko tayari kutoa ushirikiano kwa kamati ya sensa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika zoezi la sensa ya majaribio ili kuweza kusaidia serikali kutekeleza mipango yake vizuri.






Post a Comment

0 Comments