Header Ads Widget

MWANAMKE ALIYEOLEWA KWA MIAKA 9, AGUNDUA MIAKA 30 BAADAYE KUWA NI MWANAMUME

Mwanamke aliyeolewa kwa miaka 9 agundua miaka 30 baadaye kuwa ni mwanamume


Chanzo cha picha, GOPAL SHOONYA / BBC


Maisha yao yalikuwa yakiendelea kama kawaida, wenzi hao walikuwa wamejaribu kwa kila namna kutafuta mtoto.

Miezi michache iliyopita, mwanamke huyo alikwenda kwa daktari na malalamiko ya maumivu ya tumbo.


Kile alichogundua wakati wa uchunguzi kilibadilisha kabisa maisha yake milele.


Mwanamke huyo aligundua kuwa, alikuwa mwanaume, wala sio mwanamke kwa kuzaliwa, sio tu kwamba alikuwa na tezi dume ambazo hazikuonekana kwa nje lakini pia alikuwa na saratani.


Kulingana na madaktari, hii ni kwasababu ya tatizo linalojulikana kama Androgen Insensitivity Syndrome (AIS), ambalo kwa wastani humkumba mtu mmoja kati ya watu 22,000

.Ashtuka kwa kuuona mwili wa rafiki yake katika darasa la utafiti wa miili ya binadamu
'Mume wangu alikuwa malaika-kisha akanibaka'
'Nilikubali muuaji wa mume wangu anioe baada ya miaka miwili ya ndoa nikamuua kwa kulipiza kisasi'

Hali ya kutatanisha


Miezi michache iliyopita, Netaji Subhash Chandra Bose, mwanamke kutoka wilaya ya Birbhum, alifika katika hospitali ya Saratani ya Bose huko Kolkata na malalamiko ya maumivu ya tumbo.


Kulingana na ripoti ya shirika la habari PTI, mtaalam wa masuala ya vivimbe wa kliniki Dkt. Anupam Dutta na daktari wa upasuaji Soumen Das walipomchunguza, walifahamu juu ya utambulisho wake wa kweli na wakabaini kuwa na korodani kwa ndani.


Kulingana na Dkt.Dutta, "Anaonekana kama mwanamke. Sauti yake, matiti na sehemu za siri zilizostawi vizuri ni kama mwanamke wa kawaida.



Chanzo cha picha, GOPAL SHOONYA / BBC


Walakini, hana tumbo la uzazi wala kifuko cha mayai. Sio hivyo tu, hajawahi kupata hedhi".


Wakati wa uchunguzi, ilibainika kwamba alikuwa akisumbuliwa na seminoma (saratani ya tezi dume).


Kwa kawaida mwanamke anakuwa na kromosomu ya XY badala ya kromosomu ya 46 XX.


Sehemu za siri za kike pia ilipatikana kuwa njia ya uke wake ni fupi mno, imezuiwa na tishu na hivyo basi, haifiki kwenye mji wa uzazi.


Ikiwa mwanamke ana nyumba ya uzazi, tatizo hili linaweza kurekebishwa kupitia upasuaji.

Ugongwa wa AIS ni nini?


Ugonjwa huu wa Androgen insensitivity kwa kiingereza husababisha sehemu za siri za mtoto na viungo vya uzazi kutokua kikamilifu.


Mwili haujibu homoni za kiume za androjeni kwa hivyo zinakuwa na sifa sawa na wanawake.


Hali hii ndio inayotambulika kama androgen insensitivity syndrome (CAIS) Kwa ukamilifu.


Inachukua muda kugundua ugonjwa huu wa CAIS, kwani viungo vya mtoto ni sawa na vya msichana wa kawaida.


Hii inaripotiwa wakati hana hedhi akiwa ameshafikisha umri wa kubalehe, wakati nywele katika sehemu za siri au chini ya kwapa hazijitokezi.


Kadri mtoto anakua, anahitaji ushauri zaidi.


Ikiwa mwili utajitokeza kwa asilimia kidogo tu kwenye homoni ya androjeni, ugonjwa huu utatambulika kama wenye hisia kidogo tu za androjeni yaani partial androgen insensitivity syndrome (PAIS).


Katika hali hii, mtoto pia ana dalili mchanganyiko za kiume na kike.


Dalili iliyochanganyikana ni kwamba mtoto hana jinsia au ipo kwa mbali yaani kama alama tu.


Katika hali nyingine, tiba ya homoni na matibabu mengine yanaweza kubadilisha ukuaji wa sehemu za siri.


Wazazi wanaweza kufanya uamuzi juu ya hali hii kupitia ushauri wa matibabu na tiba huanza kulingana na jinsia (mwanamume au mwanamke) ile inayofaa zaidi.


Kipindi hiki, mtoto anahitaji ushauri wa akili.


Madaktari walipomchunguza dada wa mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka 28, waligundua pia naye anaugua AIS.


Mbali na hao, shangazi wawili wa mwanamke huyo pia wamegunduliwa kuwa na ugonjwa wa AIS.

Maya', mwili na hatma yako


Maya kwa sasa anafanyiwa tiba ya chemotherapy na hali yake ni ya kawaida tu.


Kulingana na Dkt. Dutta, "Alikua kama mwanamke. Ameolewa na mwanamume kwa karibu muongo mmoja. Kwa hivyo tunamshauri kama mgonjwa na mumewe. Tumemshauri kuishi maisha ya kawaida kama vile yeye anavyoishi muda huu".


Anasema, "Tezi dume mwilini mwake hazijaendelezwa, ambako hakukusababisha uwepo wa testosterone hata kidogo.


Wakati kutokana na homoni kama mwanamke, alionekana mwanamke kamili, "Testosterone ni homoni inayoamua jinsia kwa wanaume, ambayo husababisha nywele kukua kwenye miili yao na kuwafanya kuwa na sauti tofauti na wanawake. Mbali na hii, pia huunda seli za kuzaliana"
 
 
SOMA ZAIDI HAPA ;CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments