Header Ads Widget

MWALUKO AGEUKA MBOGO, KUWAFUNGIA LESENI WANAOKWEPA KULIPA MAPATO YA SERIKALI


Afisa Ustawi wa Wanyama na Mazao ya Mifugo mkoani Shinyanga Veran Mwaluko, akizungumza na vyombo vya habari.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

AFISA Ustawi wa Wanyama na Mazao ya Mifugo mkoani Shinyanga Veran Mwaluko, amewaonya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha chakula cha mifugo bila ya kukata kibali na kuikosesha mapato Serikali, kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mwaluko amebainisha hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari, akiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, kwenye Ofisi za Jeshi hilo.

Amesema kumekuwapo na ukweukwaji mkubwa wa Sheria kwa wafanyabiashara, kuacha kukata vibali vya Serikali wakati wa kusafirisha chakula cha mifugo, ikiwamo kupeleka nje ya nchi, na kuisababisha Serikali kukosa Mapato, fedha ambazo zingetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Hivi sasa tutaanza oparation ya kuwasaka wafanyabiashara wote ambao wanafanya biashara ya kusafirisha chakula cha mifugo bila ya kukata kibali, na tutakaye mkamata atatozwa faini ya Sh. milioni 1.5 au kumfungia Lesseni yake ya biashara,”amesema Mwaluko.

Katika hatua nyingine Mwaluko amewaonya wananchi wa Mkoa huo, kucha mara moja tabia ya kuchinja mifugo kwenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwamo Misiba na Harusi, bila ya kupewa kibali wala kukaguliwa na maofisa mifugo, kuwa atakaye kamatwa atatozwa Sh.500,000.

Aidha, Mwaluko amewaonya pia wananchi wa mkoa huo, kuacha kuwatesa wanyama hasa Punda kwa kuwachapa fimbo huku wakiwa na wamebeba mizigo, na kubainisha kufanya hivyo ni kukeuka sheria za wanyama.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga George Kyando, amesema watashilikiana vyema kwenye Oparationi hiyo ya kukamata watu ambao wanakeuka sheria hizo, ukiwamo kuikosesha Serikali mapato, pamoja na kulinda afya za wananchi kwa kuacha kuchinja mifugo hovyo bila ya kupewa kibali na kukaguliwa.


Afisa Ustawi wa Wanyama na Mazao ya Mifugo mkoani Shinyanga Veran Mwaluko, akizungumza na vyombo vya habari.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akizungumza kwenye kikao hicho na waandishi wa habari.

Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.














Post a Comment

0 Comments