TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

BITEKO AONYA UTOROSHAJI MADINI, ATOA MIEZI MIWILI WALIO HODHI LESSENI ZA UCHIMBAJI MADINI KUTAIFISHWA


Waziri wa Madini Dotto Biteko, akizungumza kwenye ufungaji wa maonesho ya biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga

Na Marco Maduhu, Shinyanga


WAZIRI wa madini Dotto Biteko, ameyafunga Rasmi Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, na kuwaonya wale ambao bado wanaendekeza tabia ya kutorosha madini, waache mara moja bali wayauze kwenye masoko ya madini.

Biteko ametoa angalizo hilo leo wakati akizungumza kwenye ufungaji wa Maonesho hayo, amesema Serikali haitavumilia tabia ya baadhi ya watu kuendelea kutorosha madini, bali watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Tusitoroshe madini, mimi nashaghaa tumeondoa kila aina ya vikwazo kilichokuwa kikiwafanya watu watoroshe madini, tulikuwa na mlolongo wa kodi, tulikuwa tuna chaji VAT asilimia 18, aslimia 5 na Mrahabaa, tumeondoa kodi peke yake zaidi ya asilimia 23, lakini tunaona watu kotoka nje ya nchi za Congo, Zambia na Msumbiji ndiyo wanakuja kuuza madini hapa nchini laki Watanzania wana yatorosha hebu tuweni wazalendo,” alisema Biteko.

“Laki watu ambao bado wanaendelea kutorosha madini tuwakemee, na hawatobaki salama, ni sawa na kuchoma Mahindi kwa Tochi hayotoiva, pelekeni madini kwenye Masoko ya Madini, na Tanzania nzima tuna masoko 50, na vituo vya kuuza madini 49, tuone fahari kulipa Kodi,”aliongeza Biteko.

Katika hatua nyingine alisema, wale ambao wameshikilia Lesseni za uchimbaji madini kwa muda mrefu bila ya kuziendeleza Lessen zao, zote zitafutwa ndani ya Siku 60 (Miezi Miwili),na wale ambao wanadaiwa Sh.bilioni 9 watazilipa hata kwa kupelekwa Mahakamani.

“Kama una Lesseni ya madini endeleza Lesseni yako, lazima tuheshimiane, kama huwezi watu wakipata madini kwenye eneo hilo waache ni wakati wao acha walambe lambe, hatutaki tuwasumbue wachimbaji wakubwa, laki vilevile wachimbaji wadogo wasisumbuliwe, tunaishi kwa kutegemeana, mkiona Madini yameibuliwa sehemu fulani ghafla anajitokeza mtu akidai ana Lesseni, hilo hatutaki liendelee,” alikazia Biteko.

Pia alisema Rais Samia Suluhu Hassani, alipoingia madarakani na kuwateuwa, aliwaelekeza na kuwaambia kazi kubwa waliyonayo ni kuifanya Sekta ya madini iondoe umaskini kwa Watanzania na kuwatajirisha, na kubainisha kazi hiyo siyo ndogo, sababu maeneo mengi yenye Rasilimali za madini watu wake hua ni Maskini, na kunufaisha watu kutoka nje ya nchi, vitu ambavyo vina muumiza Rais Samia.

Aidha Biteko alisema licha ya changamoto za Madini, lakini kuna mafanikio ambayo yameonekana kwenye Sekta hiyo, ambapo mchango wake umepanda kutoka asilimia 3.4 hadi 6.7, na Maduhuli ya Serikali yamepanga kutoka Milioni 168 mpaka bilioni 580, na Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka uliopita umezalisha Tani Mbili za dhahabu.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula, alikazia suala la kutaifisha watu ambao wanashikilia Lesseni za uchimbaji madini kwa muda mrefu, pamoja na kulipa fedha za Kodi ambazo wanadaiwa kwenye Lesseni hizo Sh, Bilioni 9.3, fedha ambazo zitakwenda kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, alisema Serikali mkoani humo, wataendelea kusimamia Sekta hiyo ya madini, ulikuwepo na mahusiano ya madini na ustawi wa maendeleo ya wana Shinyanga.

Alisema Maonesho hayo ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani humo, yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuutangaza mkoa huo katika fursa mbalimbali za uwekezaji, hasa kwenye sekta ya Madini na Viwanda.

Aidha, alisema kupitia maonesho hayo, washiriki wamepata fursa ya kutambulisha biashara zao, pamoja na wachimbaji wadogo, wakati, na wakubwa, kujifunza Teknolojia za kisasa, na kupata fursa za wapi wapate mitaji, na kuwa bora zaidi katika shughuli zao na kutoa mchango wao kwa Taifa.

Dk, Sengati aliongeza kuwa, Shinyanga itaendelea kuwa mfano katika Suala la Madini, na kubainisha kwa Takiwimu Mkoa huo ni watatu kuchangia uchumi nchi, na wataendelea kujipanga vizuri na wadau, ili mchango uwe mkubwa zaidi na na mwaka huu mkoa huo utakuwa wakwanza kuchangia pato la Taifa, na kuzishinda Geita na Mara.

Maonesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga. yalianza Rasmi Julai 23 mwaka huu, na kuhitimishwa leo, huku Kauli Mbiu ikisema UWEZEKAZI WA MADINI NA VIWANDA SHINYANGA KWA UCHUMI ENDELEVU.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI.


Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza kwenye ufungaji wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof, Idris Kikuli, akizungumza kwenye ufungaji wa Maonesho ya Biashara ya Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati, akizungumza kwenye ufungaji wa maonesho hayo ya Biashara na Teknolijia ya madini.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Kulwa Meshack akizungumza kwenye maoenesho hayo.

Mwenyekiti wa wachimbaji Wadogo mkoani Shinyanga (SHIREMA) Hamza Tandiko, akizungumza kwenye Maonesho hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Maonesho hayo.

Awali Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa kwenye Banda wa Tume ya Madini.

Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa ameshika madini ya Almasi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akiwa ameshika madini ya Almasi.

Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa kwenye Banda la uchimbaji Madini ya Almasi Mwadui, Wiliamson Diamond na kuangalia miamba ya madini hayo.

Waziri wa Madini Dotto Biteko, kushoto, akisiliza maelezo namna Mgodi wa uchimbaji Madini ya Almasi Mwadui Jinsi uzalishaji wake ulivyokuwa kabla ya kuufunga kutokana na Janga la Virusi vya Corona, kutoka kwa mtaalam wa madini wa Mgodi huo Shagembe Mipawa.

Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa kwenye Banda la Mgodi wa Bulynhulu

Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa kwenye Banda la uchimbaji Madini ya Dhahabu StamiGold.

Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiangalia shughuli za uchimbaji Madogo wa Madini.
Waziri wa Madini Dotto Biteko, akiwa kwenye Banda la Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira (SHUWASA) kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandis Yusuph Katopola.

Wananchi Shinyanga wakiwa kwenye ufungaji wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini.

Wananchi Shinyanga wakiwa kwenye ufungaji wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini.

Wananchi Shinyanga wakiwa kwenye ufungaji wa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Hope wakitoa burudani.

Wanafunzi Shule ya Msingi Little Treasure wakitoa burudani.

Awali Waziri wa Madini Dotto Biteko, akikagua mabanda mbalimbali kwenye Maonesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.