Header Ads Widget

WANANCHI WAMPONGEZA KATAMBI UTATUZI WA KERO NA KUWALETEA MAENDELEO


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza na wananchi wa Kitangili kwenye mkutano wa hadhara huku akiwa ameshika ilani ya uchaguzi ya CCM na kuwaeleza mikakati yake ya kimaendeleo jimboni humo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini, wamempongeza Mbunge wao Patrobas Katambi, kuwa ndani ya mfupi amewaletea maendeleo makubwa na kutatua baadhi ya kero zao.

Wananchi wamebainisha hayo kwa nyakati Tofauti kwenye Ziara ya Katambi, alipokuwa akitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara, na kuwaeleza juu ya mikakati yake ya kimaendeleo jimboni kwake.

Wamesema wana matumaini makubwa na Mbunge Katambi, ambapo amekuwa akisikia kilio chao na kukifanyia kazi, na kubainisha kuwa huyo ndiyo Mbunge waliokuwa wakimtaka Shinyanga, ambaye ana sikiliza shida za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi.

Mmoja wa wananchi Emmanuel Martin kutoka kijiji cha Uzogore, amesema kwa muda mrefu walikuwa wakilia ujenzi wa daraja ambalo lina unganisha vijiji viwili vya Uzogore na Bwagwandege, lakini kwa sasa ujenzi wa daraja hilo unaendelea.

"Tuna furahi sana kuwa na Mbunge ambaye anasikiliza shida za wananchi wake na kuzifanyia kazi, harafu siyo mtu wa kujikweza, ambapo tuna kula naye chakula hadi cha mama lishe ugali na mrenda," wamesema wananchi wa Shinyanga kwa nyakati tofauti.

Naye Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka, amesema wamefanya kazi na Mbunge Katambi kwa muda mfupi, ambapo yameonekana mabadiliko makubwa ikiwamo ujenzi wa Zahanati ya Kitangili, uchongaji wa barabara, ujenzi wa madarasa, vyoo, mitaro, na kalavati.

Kwa upande wake Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, akiwa kwenye Ziara yake ,amesema yeye siyo Mbunge wa Porojo bali ni mtu wa kazi.

Amesema ndani ya miezi sita ya ubunge wake na unaibu Waziri, ameshafanya maendeleo Shinyanga, ikiwamo ujenzi wa madaraja, kalavati, visima vya maji, vyumba vya madarasa, matundu ya choo, Zahanati, miundombinu ya barabara, pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji.

"Ndugu zangu wanashinyanga, licha ya mimi kutatua changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wangu, pia tumpongeze Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutushika mkono,na kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na Wanashinyanga mkiwemo," amesema Katambi.

"Mfano kwenye Bajeti ya mwaka wa fedha (2021-2022) ambayo tumeipitisha hivi karibuni bungeni, kuna fedha zimetolewa na Rais wetu Samia Sh. bilioni 45 ambazo zitajenga maboma ya Zahanati na Vituo vya afya 900 nchi nzima, ambapo Shinyanga tu Zahanati Nne," ameongeza.

Pia amesema kuna fedha zingine Sh.bilioni 31.2 ambazo zitajenga Zahanati 500 kwa nchi nzima, zikiwamo na fedha nyingine ambazo zitajenga miundombinu ya barabara, na kuwataka wananchi wa Jimbo hilo, kuendelea kuwa na imani na viongozi wao katika kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza na wananchi wa Oldshinyanga kwenye mkutano wa hadhara na kuwaeleza mipango ya kimaendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza na wananchi wa Kitangili kwenye mkutano wa hadhara na kuwaeleza mipango ya kimaendeleo.

Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbuge Katambi.

Wananchi wa Kitangili wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akisiliza kero za Wafanyabiashara Soko Kuu na kuahidi kuzifanyia kazi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akiwa ndani ya Soko Kuu Mjini Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akiwa katika ukaguzi wa ujenzi wa daraja ambalo lina unganishi vijiji viwili vya Uzogore na Bugwandege.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizundua moja ya mradi ambao ameutekeleza wa kisima cha maji katika shule ya Sekondari ya Kolandoto.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kitangili.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akikabidhi kiti kwa ajili ya wagonjwa katika Zahanati ya Kitangili.

Awali Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akila chakula kwa mamalishe katika Soko kuu mjini Shinyanga na kuwaunga mkono katika shughuli zao za ujasiriamali.

Katambi akiendelea kura chakula kwa Mama lishe, akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini kulia Dotto Joshua.

Katambi akicheza muziki na wananchi kwenye mkutano wake wahadhara na kufurahi nao pamoja.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.































































































Post a Comment

0 Comments