TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

MWANDISHI WA HABARI JOSEPHINE CHARLES ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA ...BONANZA LAKE LA MICHEZO KUFANYIKA AGOSTI 14Josephine Charles

Leo Julai 23,2021 Mwandishi wa Habari na Mtangazaji maarufu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Josephine Charles anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza, Josephine amesema kwa mwaka huu alikuwa amejipanga kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya Bonanza la Michezo lakini kutokana na kuwepo kwa Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga imebidi afanye sherehe ya kukata keki na marafiki zake na wadau wa vipindi vyake vya afya, na Mambo Leo.

"Nimekuwa kila mwaka nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi kwenye wodi za wazazi, ambapo mwaka 2019 nilitoa zawadi katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga na mwaka Jana nilitoa katika Hospitali ya Kolandoto.

"Mwaka huu 2021 nilikuwa nimepanga kusherehekea kwa kufanya bonanza la michezo, lakini nimeahirisha hadi Agosti 14 mwaka huu, kutokana na kuwapo na Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini," amesema Josephine.

"Asanteni wote mlionitakia matashi mema kwa kumbukizi ya kuzaliwa kwangu na mnaoendelea kunitakia heri,Naomba nitumie nafasi hii kukualika wewe rafiki,ndugu jamaa na wadau wote ambao nilishafanya nao kazi katika Vipindi vyangu pamoja na wale ambao wanatamani kufanya kazi na mimi bila kusahau wana tasnia wenzangu kukata keki pamoja na kufungua Shampein Karena Annex Hotel Mjini Shinyanga kuanzia saa mbili na nusu leo usiku,Karibu tufahamiane,Tufurahi pamoja", amesema Josephine.