Header Ads Widget

MKANDARASI MATATANI KUSHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA UMEME


Waziri wa Nishati Dk Medard Kaleman, akizungumza na wananchi.Picha na Florah Temba.


Waziri wa Nishati, Dk Medard Kaleman ameagiza kusakwa na kukamatwa kwa mkandarasi wa kampuni ya Njarita kwa madai ya kushindwa kukamilisha mradi wa Rea kwa wakati na kutokuwepo eneo la mradi.


Mbali na hilo, Waziri ametoa miezi miwili kwa kampuni tatu za usambazaji wa umeme vijijini kwa Mkoa wa Kilimanjaro, kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na umeme na kwa kampuni itakayoshindwa mkandarasi akamatwe.

Dk Kalemani alitoa agizo hilo jana Julai 29, 2021 wakati akizindua mradi wa ujazilizi awamu ya pili (2A) katika Kijiji cha Maore, Wilaya ya Same, ambapo amesema Serikali inalipa fedha nyingi kwa ajili ya wananchi kupata huduma.

Kampuni zilizopewa miezi mitatu kukamilisha miradi ya umeme ni Ubarn & Rural Engineering Services, Octopus Engineering na Njarita Contractor huku akiagiza kampuni ya Ubarn, mkandarasi akatwe asilimia 10 kutokana kuchelewesha mradi.

"Kuna kampuni nyingi Kilimanjaro, kampuni ya Njarita haijafikisha umeme kwa miaka sita na ndizo nguzo mnaziona zimesimikwa, hazina waya na wananchi hawajaunganishiwa umeme na leo haiko hapa,"alisema Waziri Kalemani.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.


Post a Comment

0 Comments