Header Ads Widget

ASASI ZA KIRAIA, MASHIRIKA WAAHIDI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA MKOANI SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Bi Zainab Telack akisisitiza jambo wakati wa Hafla fupi ya kuwapongeza na kutambua mchango wa  viongozi wanawake waliofanya vizuri akiwemo Mkuu huyo wa Mkoa na Kamanda wa Jeshi la Polisi ACP Debora Magiligimba waliohinda tuzo hivi Karibuni

 Na Josephine Charles-SHINYANGA.

Katika kutambua nafasi za viongozi wanawake Mkoani Shinyanga ambao wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, asasi za kiraia pamoja na Mashirika yanayotekeleza Miradi mbalimbali ya mapambano hayo, zimeamua kuwapongeza Mkuu wa Mkoa huo Bi Zainab Telack na kamanda wa Jeshi la Polisi baada ya  kuchukua  Tuzo kwa nyakati tofauti hivi karibuni huku wakizitumia tuzo hizo kutafakari kwa pamoja jitihada za kutokomeza ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania Mkoa wa Shinyanga Bi Glory Mbia akizungumza kwa niaba ya asasi,  amesema lengo la hafla hiyo ni kuwapongeza Viongozi wakuu Mkoani hapa waliopokea Tuzo za heshima ikiwa ni kutambua mchango wao katika masuala mbalimbali sanjali na nafasi za viongozi wanawake katika mkoa wa Shinyanga kwa ngazi zote hasa katika kupinga vitendo vya Ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Bi Glory amesema kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi  Zainab Telack amekuwa mfano na chachu kwa viongozi wengine wanawake baada ya kutwaa tuzo  wakati wa kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili  ambapo  UNFPA  kwa kushirikiana na Wadau wake iliandaa tuzo kwa machampioni 16 wa kupinga ukatili.

Aidha Bi Glory amebainisha kuwa tuzo ya pili ni ile iliyokwenda kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP.Debora Magiligimba baada  ya kushinda tuzo katika   kategori ya Mwanamke kinara katika Taasisi za umma kanda ya ziwa na kuibuka Mshindi ambapo ni mwanamke ambaye anaongoza taasisi kubwa yenye kuhakikisha ulinzi na usalama wa watanzania unaimarika.

Awali akifungua hafla hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mlezi wa Asasi za Kiraia Mkoani hapa Bw. Thedson Ngwale  amesema Shinyanga ina  kila sababu ya kujivunia viongozi wanawake kwa sababu hali imekuwa tofauti na miaka ya nyuma, kutokana na kukithiri kwa matukio mengi ya unyanyasaji na ukatili,lakini uwepo wa viongozi hao umesaidia kwa kiwango kikubwa   hali ambayo inatia matuamaini.

hata hivyo Ngwale  amezipongeza asasi za kiraia zote zilizoamua kuungana pamoja kuandaa hafla hiyo ya kutambua na kuwapongeza Viongozi wanawake Shinyanga kwani inaleta hamasa zaidi kufanya kazi na hasa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia  na kutaraji kuona mabadiliko makubwa zaidi miaka mitano mbele endapo Viongozi hawa wataendelea kuwepo.

Mussa Ngangala ni Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mkoani Shinyanga ameiomba Serikali ya mkoa  huu kutenga dawati maalumu kwa ajili ya kusikiliza na kupokea kero za wadau pamoja na asasi za  kiraia pale wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mussa ameongeza kwa kusema kuwa wadau wote wa Masuala ya Ukatili wanaipongeza ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaoutoa hususani muda wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya kuhakikisha ukatili unatokomezwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Afisa Miradi Kutoka PACESHI John Shija ameomba Maboresho yafanyike katika uendeshaji wa Kesi za ukatili wa Kijinsia kwa Jeshi la Polisi na Mahakama ili kudhibiti ushahidi usipotee na kupelekea kesi kufutwa, kwani  kufanya hivyo jamii itapata hofu na kuacha kutenda vitendo vya ukatili wa kijinsia endapo wataona na kusikia hukumu inatolewa dhidi ya watenda makosa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Investing in Children and their Societies (ICS) Bw. Kudely Sokoine amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kuwakutanisha na wadau wanaoshughulikia masuala ya Afya pamoja na  Wadau wanaoshughulikia masuala ya Ukatili wa Kijinsia kwa kuwa yana Uhuasiano wa karibu katika kupunguza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha moja wakati wa utekelezaji wake.

 Jonathan Manyama  Mkurugenzi wa Asasi ya thubutu Africa Initiatives  amesema asasi za kiraia kuna wakati wananyong’onyezwa na baadhi  ya ofisi za Serikali pale wanaombwa fedha  kwa ajili ya kuchangia shughuli za kiserikali na kushindwa kuchangia kulingana na hali iliyopo hushindwa kutambulika,hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa kama Mama kuwa akiona watoto wake hawana pesa muda huo awaelewe asiwatenge.

Sabrina Majikata yeye ni Meneja Miradi kutoka ICS amesema hivi karibuni Mkoa umezindua  Mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini kigumu walichonacho katika asasi hizo ni kutafuta fedha ya kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili lakini  changamoto wanayaokumbana nayo ni upatikanaji wa Takwimu sahihi.

Sabrina ameomba kupatikana muafaka wa Takwimu Sahihi na zinaznoendana na wakati  zinapohitajika ili kuondoa ile hali ya kila Taasisi kuwa na Takwimu zake Mfano Polisi kuwa na Takwimu zake,Ofisi ya Ustawi wa Jamii kuwa na Takwimu zake.

ACP Debora Magiligimba akiuzngumza katika hafla hiyo amezipongeza asasi za kiraia mkoani Shinyanga kwa kazi nzuri wanayofanya huku akibainisha kuwa ataendelea kushirikiana nao katika mapambano ya ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ili jamii ya mkoa wa Shinyanga iweze kuishi kwa  amani.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack amezishukuru asasi hizo kwa Pongezi nyingi baada ya kuandaa hafla  ya kuwapongeza wanawake Viongozi Mkoa wa Shinyanga kwa kazi wanazofanya ambapo amehaidi kuedelea kushirikiana na kutatua kero zote zinazowakumba wanachi .

amesema Tuzo aliyoipokea siyo yake tu bali niya Shinyanga nzima kwa kuwa hawezi kufanya kazi peke yake bila wadau wa maendeleo.

Kuhusu Changamoto na maombi yaliyosemwa na wadau wote wa Asasi za Kiraia amesema anaenda kuyafanyia kazi maombi yote yaliyotolewa na wadau hao wa kupinga ukatili wa kijinsia.

aidha,Viongozi wengine wanawake waliotambuliwa katika hafla hiyo ,Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Elizabeth Mbezi,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba,Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kanda ya Shinyanga Mhe. Mary Mrio,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba,Hakimu wa Wilaya Mhe. Ushindi Swalo na Wabunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP. Debora Magiligimba akizungumza wakati wa hafla fupi  iliyoandaliwa na asasi za kiraia Mkoani Shinyaga kutambua mchango wa viongozi wanawake aionyesha kitabu cha Mpango Mkakati wa kutokomeza ukatili.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Telack ,akizungumza wakati wa hafla fupi  iliyoandaliwa na asasi za kiraia Mkoani Shinyaga kutambua mchango wa viongozi wanawake pamoja na tuzo aliyoipata wakati wa siku 16 za kupinga ukatili.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP. Debora Magiligimba akizungumza wakati wa hafla fupi  iliyoandaliwa na asasi za kiraia Mkoani Shinyaga kutambua mchango wa viongozi wanawake.
Bi Glory Mbia Mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania(WFT)akieleza sababu zilizosababisha Asasi za kiraia Mkoani Shinyanga Kuandaa hafla hiyo ya kuwapongeza viongozi wanawake walioshinda tuzo mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa  na Kamanda wa Polisi.

Jonathan Manyama  Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Thubutu Africa Initiatives akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel.
Sabrina Majikata  Meneja Miradi kutoka ICS akisisitiza juu ya suala la upatikanaji wa takwimu sahihi zinazohusiana na masuala ya ukatili.
Bw John Shija Mkurugenzi wa Shirika la Msaada wa kisheria Mkoani Shinyanga akieleza masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuwapongeza viongozi wanawake Mkoani Shinyanga.
Mussa Ngangala, Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mkoani Shinyanga akiomba Serikali ya mkoa  huo kutenga dawati maalumu kwa ajili ya kusikiliza na kupokea kero za Wadau wa Masuala ya ukatili.
Mkurugenzi wa  shirika la  Investing in Children and their Societies (ICS) Bw. Kudely Sokoine akisisitiza jambo kwenye  hafla hiyo.
Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mlezi wa Asasi za Kiraia Bw. Thedyson Ngwale akieleza masuala yanayosimamiwa na kutekelezwa na Idara yake.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Jasinta Mboneko akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo.

wakiwa katika picha ya Pamoja  Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack,akifuatiwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Bi Elizabeth Mbezi pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiliimba.

Wa Pili Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Shinyanga Bi Magreth Ndaweka akiwa na baadhi ya Washiriki wa hafla ya kuwapongeza Viongozi wanawake Mkoani hapa.
Washiriki wakiendelea kufuatilia hotuba na nasaha za Viongozi mbalimbali 
Washiriki wakiendelea kufuatilia hotuba na nasaha za Viongozi mbalimbali.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja 
Mussa Ngangala Mkurugenzi wa TVMC  kushoto akiwa katika pich ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Pacesh Bw John Shija 


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Sinyanga Dkt.Yudas Ndungile akiwa ameketi meza moja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack.























Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba akikata keki pamoja na Mkuu wa Mkoa  Mheshimiwa Zainab Telack .














 


Post a Comment

0 Comments