Header Ads Widget

SAKATA LA MAUAJI YA MLELWA, DPP AIDHINISHA MASHTAKA YA MAUAJI KWA WATUHUMIWA 4

  

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Biswalo Mganga

Na Shinyanga Press Club Blog

Leo Septemba 30, 2020 Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Biswalo Mganga ameidhinisha mashtaka ya mauaji ya kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2019) dhidi ya watuhumiwa THADEI WALTER MWANYIKA, GEORGE SANGA, OPTATUS NKWERA na GOODLUCK OYGEN MFUS wanaotuhumiwa kumuua aliyekuwa Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) vyuo vikuu mkoani Njombe, Emmanuel Mlelwa.

DPP Mganga ametoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya habari, ambapo ameeleza kuwa ushahidi unaonyesha uhusika wa watuhumiwa wengine ambao bado hawajakamatwa. hivyo, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Usimamizi wa Mashtaka nchini, ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuendelea kufanya upelelezi ili kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wote ambao wamehusika na mauaji hayo.

"Nimeidhinisha mashtaka ya mauaji ya kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu dhidi ya watuhumiwa Thadei Mwanyika, George Sanga, Optatus Nkwera na Goodluck Mfuseba 

"Kama msimamizi wa haki jinai kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa wito kwa watu wote kuishikwa amani, utulivu namshikamano, na kwa kufuata sheria zanchi yetu. Niwakumbushe wananchi wote kuwa kutunza amani na usalama wa Taifa letu ni jukumu la kila mmoja wetu na hivyo sote tunatakiwa kufichua na kutoa taarifa juu ya vitendo vyenye mwelekeo wa kuvuruga amani na usalama wanchi yetu," amesema.

Akizungumzia tukio la mauaji hayo, Biswalo amesema mnamo Septemba 21, 2020 majira ya saa 9.30 jioni, mwili wa marehemu ambaye kwa wakati huo hakutambuliwa ulikutwa katika maeneo ya Bwawa la Kibena Estate kwenye daraja la Mtege Kata ya Ramadhani Wilaya na Mkoa wa Njombe.

Ambapo taarifa za tukio hilo zilifikishwa katika Kituo cha Polisi Njombe, kisha hatua za kuhifadhi mwili huo hospitalini zilifanyika na uchunguzi wa chanzo cha kifo ulifanyika mara moja na Daktari aliyefanya uchunguzi huo alibainisha chanzo cha kifo cha mtu huyo ambaye baadaye alitambuliwa kwa jina la Emmanuel Polycup Mlelwa, kuwa ni ukosefu wa hewa (Suffocation). 

"Jeshi la Polisi lilifanya upeleleziwa tukio hilo la mauaji ikiwa ni pamoja na juhudi za kuwasaka wahusika. Kutokana na upelelezi huo,walikamatwa watuhumiwa wanne, THADEI WALTER MWANYIKA,GEORGE SANGA, OPTATUS NKWERA na GOODLUCK OYGEN MFUSE.

"Baada ya upelelezi wa awali wa shauri hili  kukamilika, Jeshi la Polisi liliwasilisha jalada kwangu kwa ajili ya kulisoma na kufanya uamuzi juu ya uwepo au la wa ushahidi unaokidhi kufungua mashtaka dhidi ya watuhumiwa kwa mujibu wa sheria," amesema. 

 Taarifa hiyo ya Biswalo iliendelea kubainisha kuwa mara baada ya kufanya mapitio ya ushahidi uliokusanywa, alibaini kwamba mtuhumiwa THADEI WALTER MWANYIKA mkazi wa Kambarage Njombe mjini na Mgombea nafasi ya udiwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu wa 2020 katika kata ya Utalingolo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) baada ya kukamatwa na kupewa onyo (caution) sambamba na haki zake kwa mujibu wa sheria, alieleza kuwa mnamo Septemba 20, 2020 majira ya saa tano (5.00) usiku alimuita EMMANUEL POLYCUP MLELWA (ambaye sasa ni marehemu) kwenye bar iitwayo Tale iliyopo Njombe Mjini na kisha walimteka. 

"Mtuhumiwa anawataja baadhi ya walioshiriki katika utekaji huo kuwa ni GEORGE SANGA, ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia naMaendeleo (CHADEMA) Jimbo la Njombe Mjini, OPTATUSNKWERA ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ramadhani na GOODLUCK OYGEN MFUSE, mkazi wa Njombe Mjini," amesema.

 Pia alibaini kuwa watuhumiwa wote walieleza kwamba baada ya kumteka walimuingiza kwenye gari aina ya GAIA rangi ya fedha (silver) yenye namba za Usajili T. 457 DAB na kumpeleka kwenye eneola bwawa la Kibena Estate ambapo walimtesa na baadaye kumnyonga na kisha kumtupa ndani ya bwawa hilo.

"Mtuhumiwa GEORGE SANGA alipopekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na fulana (T-shirt) mbili za CHADEMA, moja ikiwa na matone ya damu, gari aina ya GAIA rangi ya fedha (silver) yenye namba za Usajili T. 457 DAB na mkanda wa suruali ya EMMANUEL POLYCUP MLELWA (Marehemu) ambao watuhumiwawanaeleza kuwa waliutumia kumnyonga mpaka kufa.

"Nimepitia kwa makini ushahidi niliourejea kwa ufupi hapo juu na kujiridhisha kuwa unatosha kufungua mashtaka dhidi ya watuhumiwa tajwa. Hivyo basi, baada ya kuzingatia misingi iliyoanishwa katika Ibara ya 59 B (4)(a) hadi (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na masharti ya Sheria ya Usimamizi wa Mashtaka Na.28 ya mwaka 2008, leo Septemba 30, 2020 nimeidhinisha mashtaka ya mauaji ya kukusudia," amesema.




Post a Comment

0 Comments