TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MASWA MAGHARIBI KUPITIA (ADA TADEA) LYDIA MBUKE AAINISHA VIPAUMBELE VYAKE


Wa pili toka Kushoto ni Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama  Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akimkabidhi baadhi ya Nyaraka mgombea  ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera ili  atakapopata ridhaa ya wapiga kura akatekeleze kwa vitendo. 

Mgombea Ubunge jimbo la Maswa Magharibi kupitia chama cha ADA TADEA  Bi Lydia Mbuke Bendera amesema kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwawakilisha wakazi wa  jimbo hilo atahakikisha anatimiza  vipaumbele vyake kumi ikiwemo upatikanaji wa  fulsa  mbalimbali za ajira kwa vijana pamoja na tatizo la maji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni Jimbo la  Maswa Magharibi  katika kata ya Malampaka Mgombea huyo amesema kuwa kumekuwapo na changamoto kubwa ya tatizo la ajira nchini hususani kwa kundi kubwa la vijana.

“Suala la Ajira litakuwa ndoto kwa wana Maswa Magharibi kama mkinipatia mimi nafasi ya kuwawakilisha  na kuwapigania bungeni kwani mimi niko makini kwenye utafutaji wa fulsa za uwekezaji zitakazosaidia kupunguza tatizo la ajira me nawahakikishia tutakwenda wote bega kwa bega  hususani kwa vijana wa darasa la saba,kidato cha nne na vyuo vya kati wataweza kuendesha maisha yao”

Lydia ameongeza kuwa iwapo ataingia bungeni atapambana kadri ya uwezo wake kubuni fulsa za biashara kwa wakazi wa malampaka na jimbo zima la Maswa Magharibi ili wananchi waweze kufanya biashara kulingana na maeneo yao huku akiahidi kuboresha sekta binafsi kwa kushirikiana na wakazi wa jimbo hilo,kuunganisha jimbo lote kwa miundombinu ya barabara, kuweka mfumo rafiki wa kupokea changamoto za wananchi wake pamoja na kusimamia ujenzi wa hospiatal kutokana na uchache wa vituo vya afya.

“Kwa hiyo ndugu zangu wana Malampaka na Jimbo zima la Maswa Magharibi nina amini haya yote yanawezekana mkinipa fulsa ya kwenda jijini Dodoma kuwakilisha hizi hoja itakuwa rahisi na vyepesi kwa sababu shida zenu nyingi nazifahamu hivyo kuweni na imani na mimi ndugu zangu hakikisheni tarehe 28 mwezi wa kumi hamfanyi makosa”

Kwa upande wake Mgombea udiwani kata ya Malampaka kupitia ADA TADEA Charles Mwinuka amewaomba wakazi wa kata hiyo kumpatia kura zitakazosaidia yeye kwenda kuwawakilisha kwenye baraza la madiwani ambapo amehaidi kuanza na kero kubwa na muda mrefu ya kero maji, barabara na umeme

“Ukiangalia kwa sasa watoto wadogo   unawakuta kwenye Malambo ya maji akienda kutafuta maji ili hali huu ni mji mkongwe wa muda mrefu sana ambao ulipaswa kuwa na huduma za maji toka ziwa Victoria,angalia barabara zetu hazilingani na mji huu kwa hiyo nipeni nafasi nikawatete kwenye halmashauri huko”

Naye Mgombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita ADA TADEA Mh John Shibuda amewataka wakazi wa jimbo la Maswa Magharibi kuchagua viongoiz ambao ni sikio  la wananchi wanaosikiliza na kutatua kero zao ambao wanatoka  katika chama chake

“Najua Mnajua maana ya uongozi  mbovu ninaomba muelewe ninapowaambia kuwa ukiwa na mbunge ambaye siyo sikio la wanachi ni changamoto tu, pale ambapo tuliwahitaji  wao hawakutuitaji,tusipowahitaji wao ndo wanatuhitaji hii ndiyo shida ya kuwa na wabunge wasio kuwa sikio la  wananchi”

Mheshimiwa Shibuda amemtaka Mgombea huyo wa nafasi ya ubunge iwapo atapata ridhaa ya wananchi hakikisheni anakwenda kusimamia na kukamilisha yale yote ambayo yeye wakati akiwa mbunge wa jimbo aliyaanzisha ikiwemo ujenzi wa mabwawa ya maji yatayosaidia kukabiliana na majanga ya ukame na uharibifu wa mazingira

Mheshimiwa Shibuda amebainisha kuwa jimbo la Maswa Magharibi bado linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya wafugaji, kilimo cha zao la pamba,umeme kwa baadhi ya vijiji kutokuwa na nishati hiyo na kuchangia wananchi kushindwa kwenda na wakati wa sasa wa sayansi na teknolojia

“Wakati nikiwa Mbunge wa jimbo hili kabla ya kuwania Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliacha jimbo hili la Maswa Magharibi likiwa  asilimia 95 za huduma ya umeme yaani sehemu kubwa ya vijiji vyake vina umeme lakini leo kuna vijiji havijapata umeme mpaka leo ambayo ni sawa na asilimia 5  kwa hiyo mgombea wangu nakukabidhi barua na maadishi ya wapi nilihishia ili nawe uanzie hapo”
 Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama  Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwa ameketi  pamoja na Mgombea  ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera wakiendelea kutazama burudani zinazoendelea. 
  Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama  Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwa ameketi  pamoja na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na Mgombea  ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera wakiendelea kutazama burudani zinazoendelea. 
 Baadhi ya Machifu wa kabila la kisukuma wakiwa wameketi kwa pamoja wakiendelea kuteta jambo juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 
Baadhi ya wakazi wa kata ya Malampaka Jimbo la Maswa Magharibi wakiwa wamesimama wakiendelea kusikiliza hoja za wagombea toka (ADA TADEA) 
 Watoto nao hawakuwa mbali kusikiliza sera za wagombea waliofika kunadi katika eneo la Malampaka wakiwa na wazazi wao kwa pembeni ili kuhakikisha  wanapatikana viongozi bora na makini 
Mgombea  ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera akielekea jukwaani kunadi sera zake huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho katika mkutano uliofanyika Malampaka.
  Wananchi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea 

 Wa pili toka Kushoto ni Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama  Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda 
akimsisitizia jambo  mgombea  ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera ili  atakapopata ridhaa ya wapiga kura akatekeleze kwa vitendo awe mfano wa kuigwa na jamii ili atakapoondoka awe ameacha alama. 
 Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama  Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwakumbusha wapiga kura kuwa siku ya uamuzi sahihi ni octoba 28 mwaka huu 
Baadhi ya Machifu wa Kabila la Wasukuma wakiwa katika mkutano wa  wa wagomea Urais na Ubunge Kutoka ADA TADEA  katika kata ya Malampaka jimbo la Maswa Magharibi  
Baadhi ya Machifu wa Kabila la Wasukuma wakiwa katika mkutano wa  wa wagomea Urais na Ubunge Kutoka ADA TADEA  katika kata ya Malampaka jimbo la Maswa Magharibi  

 wananchi wakiendelea kusilikiza hoja wa wagombea 
 Mmoja wa Wagombea wa Ubunge Kupitia ADA TADEA akimnadi Mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi