TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

MBWANA SAMATTA AONDOKA ASTONVILLA, ATUA UTURUKI

Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na Club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England, bado Fenerbahce haijaweka wazi kama wamemsajili kwa mkopo wa msimu mzima 2020/21 kama inavyoripotiwa au ni uhamisho kamili

Fenerbahce wamempa jezi namba 12 Mbwana Samatta ambaye anaenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho, club hiyo imewahi kumuwania mara kadhaa hata kabla ya kwenda Aston Villa lakini ndoto ya Samatta ilikuwa ni kucheza EPL. 
 
Hata hivyo vyanzo vingine vya habari akiwemo Mwandishi nguli Salim Kikeke vimeeleza kuwa Fernabache wametangaza kumsajili Samatta kwa mkataba wa miaka minne, huku Wawakilishi wa Mbwana Samatta wakieleza kuwa usajili huo ni usajili mkubwa kufanyika katika dirisha hili la usajili nchini Uturuki.

Mbwana Samatta akiwa na wawakilishi wake pamoja na viongozi wa klabu ya Fenerbahçe S.Kni baada ya kukamilisha usajili wake