TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

ACT-WAZALENDO 'YAJICHOMOA' MBIO ZA URAIS TANZANIA, YAMPA BARAKA LISSU


Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akiwa na Aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo Bernard Membe.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo taifa, Maalim Seif Sharrif Hamad amemuidhinisha mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumzia hatua hiyo, Naibu Katibu wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Janeth Rite amesema kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa katika mkutano wake wa kampeni katika Jimbo la Donge aliweka wazi suala hilo.

"Saa chache zilizopita, Mwenyekiti wa Kitaifa wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad amemuidhinisha Tundu Lissu na hayo ni matokeo ya mazungumzo ya chini chini yaliyokuwepo kati yetu na CHADEMA, hivyo hayo ndiyo maridhiano yetu", amesema Janeth.