Header Ads Widget

WANAUME WANAONYONYA MAZIWA YA WAKE ZAO KUKATA POMBE WAONYWA


 Baadhi ya akina mama waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika Halmashauri ya Shinyanga yaliyofanyika leo Agosti 7, 2020 katika Kata ya Mwalukwa

Na Shinyanga Press Club Blog

WANAUME wameonywa na kutakiwa kuacha tabia ya kunyonya maziwa ya wake zao ambao bado wako kwenye muda wa kunyonyesha watoto, kwani vitendo hivyo huwasababishia madhara watoto wachanga ikiwemo udumavu na utapiamlo.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 7, 2020 wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya unyonyeshaji kwa Halmashauri ya Shinyanga mkoani Shinyanga ambayo yamefanyika katika Kata ya Mwalukwa.
  
Akieleza changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kutoa elimu ya unyonyeshaji kwa akinamama wilayani humo, Afisa Chakula na Lishe wa Wilaya ya Shinyanga, Said Mankirigo amebainisha kuwa watoto hukosa maziwa ya kutosha kutokana na baadhi ya wanaume kunyonya maziwa yote wakidai kuwa wanapunguza kilevi baada ya kunywa pombe.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Shirika la RAFIKI-SDO la Mjini Shinyanga linalo jihusisha na ulinzi wa mtoto, huku Afisa Mchumi Muwezeshaji kutoka shirika hilo, Ahsante Selu amesema ni vyema wanaume na wanawake wakaendelea kuelimisha juu ya unyonyeshaji wa watoto ili kumaliza changamoto hiyo.
 
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngassa Mboje akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji

 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mameritha Basike akieleza mipango mbalimbali waliyoweka kuhamasisha wanawake kunyonyesha

  Afisa Chakula na Lishe wa Wilaya ya Shinyanga, Said Mankirigo akieleza namna wanaume wanavyo kwamisha jitihada za wanawake kunyonyesha watoto
 
 Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi
 
 Mmoja wa akina mama waliohudhuria maadhimisho hayo akielezea namna alivyofanikiwa kunyonyesha vizuri watoto wake sita.