Header Ads Widget

SH MILIONI 715 ZAKARABATI NYUMBA ZA MA-DC LUSHOTO NA KOROGWE


Muonekano wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mara baada ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha Ofisi na mkazi ya viongozi.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
Shilingi milioni 715 zimetumika kukarabati Nyumba za Wakuu wa Wilaya za Lushoto na Korogwe, kujenga nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto na Ofisi nane za tarafa katika Wilaya hizo.

Ujenzi na ukarabati wa nyumba na ofisi hizo ni sehemu ya utekelezaji wa azima Serikali ya awamu ya tano kuboresha mazingira ya kazi kwa viongozi nchini.

Hayo yamebainika wakati wa makabidhiano ya nyumba na ofisi hizo katika wilaya za Lushoto na Korogwe mkoani Tanga kati ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Mabughai na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga.

Akikabidhi majengo hayo yaliyojengwa na kukarabatiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema makazi na ofisi bora ni chachu kwa viongozi kufanya kazi kwa bidii.

Dkt. Jingu amesema Chuo cha Maendeelo ya Jamii na Ufundi Mabughai kimejikita zaidi katika kuhakikisha kinaleta tija na kutoa mchango wake katika maendeleo na kuongeza ufanisi na hivyo, wataendelea kushirikiana na wadau mablimbali katika kutekeleza miradi mbalimbali.

“Niseme tu muda si mrefu tutaanzisha Kampuni ya Ujenzi kama ilivyo Suma JKT ili tuongezee nguvu zaidi ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kiwango kikubwa zaidi” alisema

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Judica Omary amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuboresha makazi na ofisi za viongozi ili kuweka mazingira mazuri ya uwajibikaji wa viongozi hao katika kuwahudumia wananchi wao.

“Rais John Magufuli amedhamiria kuboresha mazingira ya makazi na Ofisi za viongozi ili tuweze kumsaidia kutatua changamoto zainazowakabili wananchi,” alisema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika amekishukuru Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai kwa kukarabati nyumba yake kawa kikwango cha juu.

“Nasema huu si ukarabati bali wamejenga upya kwani kila kitu kimebadilika ukiangalia picha za zamami utasema imejengwa na sio kukarabati,” alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kisa Gwakisa amekiri ukarabati wa nyumba hiyo umekidhi viwango na kuwapongeza kuwa Chuo cha Mabughai kwa kazi nzuri na kuahidi kuendelea kushirikiana nacho katika kutekeleza miradi mingine Wilayani humo.

Nakiri nimeridhika na ukarabati huu ukipita nje ya nyumba hii utadhani hoteli ya kitalii vile kumbe ni nyumba ya Mkuu wa Wilaya inaopendeza sana” alisema

Awali akitoa maelezo ya miradi ya ujenzi na ukarabati wa ofisi na nyumba za viongozi mkoani Tanga uliofanywa na Chuo cha Mabughai, Mkuu wa Chuo hicho, Aidan Felix amesema chuo kimeshirikisha jamii kwa karibu katika kutekeleza miradi hiyo kwa kutumia mafundi na wataalam kutoka katika maeneo husuka hivyo kuifanya miradi hiyo kuwa ya wananchi.

Ukarabati wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Lushoto umegharimu zaidi ya shilingi milioni sitini na mbili, nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe zaidi ya shilingi million 106, na ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto umegharimu zaidi ya shilingi million 231 na ofisi nane za tarafa zimegharimu Millioni 315.

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Judica Omary (Katikati)) akikata utepe kuashiria kupokea nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto iliyokarabatiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Judica Omary wakitia saini hati za makabidhiano ya nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na Ofisi nne za Tarafa zilizokarabatiwa na kujengwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. January Lugangika (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kushoto) wakiangalia picha za munekano wa zamani wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto kabla ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (wa pili kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary hati ya kukabidhi Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto kwa baada ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary (wa pili kushoto) wakionesha hati ya makabidhiano ya Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya kufanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kisa Gwakisa wakiangalia nyumba ya Mkuu wa Wilaya huyo iliyofanyiwa ukarabati na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Aidan Felix.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Mabughai Aidan Felix (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa (kulia) kuhusu ukarabati wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe uiofanywa na Chuo chake wa pili kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judica Omary.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW