Header Ads Widget

MWINYI ZAHERA ATUA GWAMBINA FC YA MISUNGWI, NYOTA YANGA WATAJWA KUMFUATA

Mmiliki wa timu ya Gwambina FC ya Misungwi, Alexander Mnyeti (kulia) akimtambulisha kocha mpya wa timu hiyo, Mkongomani Mwinyi Zahera kwa mkataba wa miaka mitano.

MWINYI Zahera, ametambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu huu wa 2019/20 na itashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/21.


Zahera aliwahi kuifundisha Yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa.

Kocha huyo amesaini dili la miaka mitano na inaelezwa kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga.

Wanaotajwa kuibukia Gwambina ni pamoja na Mrisho Ngasa, David Molinga na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru baada ya kuachwa na Yanga.