Header Ads Widget

MTOTO WA MIAKA SITA ASHAMBULIWA NA FISI NA KUPOTEZA MAISHA


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba

Na Shinyanga Press Club Blog

Mtoto mwenye umri wa miaka sita  anayeitwa  Kulwa Machia amefariki dunia baada ya kung’atwa na fisi usoni na kujeruhiwa vibaya, wakati akitoka kuchunga mifugo akirudi nyumbani akiwa na watoto wenzake .

Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:00 jioni katika Kitongoji cha Relini Mtaa wa Nhelegani  Tarafa ya Shinyanga Mjini Manispaa ya Shinyanga,ambapo fisi huyo alimvamia mtoto huyo na kumng’ata usoni kisha kutokomea vichakani baada ya kusikia mayowe ya watoto waliokuwa na marehemu.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amesema matukio ya fisi kujeruhi na kuwaua watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi Mkoani Shinyanga yamekuwa yakiripotiwa mengi na amewataka wazazi na walezi kuchukuwa tahadhari hasa kipindi hiki.