Header Ads Widget

MRISHO MPOTO AANZA KUVAA VIATU BAADA YA KUCHOKA KUHUSISHWA NA UCHAWI


 
 
  Msanii wa mashairi Tanzania, Mrisho Mpoto katika muonekano akiwa amevaa viatu

Msanii wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto "Mjomba", ameshea picha mitandaoni ikimuonesha akiwa amevaa viatu huku akiuliza mashabiki zake kwamba aendelee kuvaa viatu au abaki kuwa peku.

Katika picha hiyo ambayo amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ameshaitwa mchawi, mshirikina kwa sababu ya imani yake ya kutembea peku.

"Nimeitwa mchawi, mshrikina na masharti ya mganga kwa kutembea peku, hapo je nirudi peku au nibaki huku" ameandika Mrisho Mpoto.

Ikumbukwe tu msanii huyo alijizolea umaarufu kutokana na style ya kutembea peku popote pale utakapomuona iwe mtaani, studio, mikutano hata akiwa stejini akifanya show na shughuli zingine za kimuziki.
 Mrisho Mpoto akitembea bila kuvaa viatu miguuni