Header Ads Widget

JAJI MKUU PROF. JUMA AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA KUU SHINYANGA, ATOA NENO KWA MAHAKIMU




Muonekano wa Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga lililozinduliwa leo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma amewataka Mahakimu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, kutenda haki kwa wananchi wote bila ya ubaguzi wa kujali hali zao wakati wa usikilizaji wa mashauri mahakamani.

Amebainisha hayo leo wakati akizundua rasmi Jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, ambalo lilijengwa mwaka 2006 na kukamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi bilioni 4.

Amesema jengo hilo limejengwa kwa madhumuni ya kutoa huduma kwa wananchi wote bila ya kujali hali zao, na kusiwepo na ubaguzi wakati wa usikilizaji wa mashauri, pamoja na uhairishaji wa mashauri hayo bila ya sababu za msingi.

“Jengo hili la mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga limejengwa kwa ajili ya kusogeza huduma kuwa karibu na wananchi, na mahakama siku zote hua ni mali ya wananchi, hivyo naomba haki itendeke kwa wote wakati wa usikilizaji wa mashauri bila ya kujali hali zao,” amesema Prof Juma.

Naye Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Othmani Chande, amesema Jengo hilo liwe msaada kwa wananchi kusikilizwa mashauri yao ya rufaa kwa wakati na kusitokee changamoto tena ya kuchelewa kusikilizwa, ili kuondoa utofauti wa zamani na kuonekana faida ya kujengwa mahakama hiyo kuu ya rufaa kanda ya Shinyanga.

Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu, amesema ujenzi wa jengo hilo ulilianza mwaka 2006 na kukamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amepongezwa uwepo wa jengo hilo ambalo litaleta manufaa kwa wakazi wa Shinyanga na mikoa jirani kuliko hali ilivyokuwa zamani, ambapo walilazimika kusafiri kwenda jijini Mwanza kupata huduma hiyo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
 

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma (katikati) akikata utepe kuzindua Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga. Kushoto ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Othmani Chande na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
 
 Zoezi la ufunguaji jiwe la msingi ukiendelea
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma, akizungumza kwenye uzinduzi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga leo Agosti 7, 2020
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Othmani Chande, akizungumza kwenye uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo
 Msajili Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilbard Chuma akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mathias Kabundugusu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemi akizungumza kwenye hafla hiyo
Mahakimu na mawakili wakiwa kwenye uzinduzi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Mahakimu na mawakili wakiwa hafla ya uzinduzi wa engo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Mahakimu na mawakili wakishuhudia uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Watendaji wa mahakama wakiwa kwenye uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga leo Agosti 7, 2020.
Watendaji wa mahakama wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Wadau wa mahakama wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahimu Juma akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Othmani Chande akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.
Picha ya pamoja.

Picha na Marco Maduhu na Shinyanga Press Club Blog