TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440

SALOME MAKAMBA APITISHWA RASMI KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI, MAJINA MENGINE YAANIKWA HADHARANI


Salome Makamba akiwa bungeni

Leo Agosti 12, 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya pili ya majina 37 ya wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali nchini.

Miongoni mwa waliopeta katika mchakato huo ni Salome Makamba aliyepitishwa rasmi kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga.

Salome alikuwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kwa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo alishinda kwenye mchakato wa kura za maoni mapema mwezi Julai, 2020.

Soma zaidi majina hayo hapa chini