Header Ads Widget

BAADA YA BERNARD MORRISON KUTUA SIMBA, YANGA YAWATULIZA MASHABIKI YADAI BADO NI MALI YAO


Bernard Morrison akisaini mkataba leo Agosti 8, 2020 wa kuanza kuitumikia Klabu ya Simba SC akitoka kwa watani wa Jadi, Yanga

Na Damian Masyenene, Shinyanga Press Club Blog

LEO Agosti 8, 2020 Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameanza kutambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili kwa ajili ya kuwaongeza kikosini kwa maandalizi ya msimu mpya na michuano ya kimataifa.

Simba wameanza utambulisho huo saa 8 mchana kwa kuweka wazi juu ya kumnasa aliyekuwa mchezaji wa Yanga SC, Mghana Bernard Morrison ambaye amekuwa akisumbua vichwa vya mashabiki wa soka nchini juu ya mustakabali wake kutokana na maelewano mabovu na mabosi wake wa zamani.

Morrison ametua Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili.

Sasa baada ya utambulisho huo, Uongozi wa Yanga ambao siku zote umekuwa ukiwaaminisha wapenzi na mashabiki wake kuwa Bernard Morrison ni mali yao na ameongezewa mkataba mpya, masaa machache baada ya kuanikwa hadharani na watani wao wa jadi, Yanga imewatuliza mashabiki wake na kwamba inalifuatilia kwa umakini suala hilo kwani bado liko mikononi mwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Jumatatu Agosti 10, 2020 litasikilizwa.

Soma zaidi hapa chini Taarifa ya Yanga SC