Header Ads Widget

ALIYEKUWA AFISA ELIMU KWIMBA ATEULIWA KUWA DED WA KISHAPU

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli
 
Leo Julai 7, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amefanya uteuzi mwingine akimteua Lauteri John Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe na kuteua wakurugenzi watano wa halmashauri.
 
Kati ya wakurugenzi wapya walioteuliwa yumo Emmanuel Matinyi Johnson ambaye anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, ambapo kabla ya uteuzi huo, Johnson alikuwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
 
Tazama majina ya Wakurugenzi wengine walioteuliwa na vituo vyao vya kazi.